Ernesto Guevara au Che Guevara (Rosario, Argentina, 14 Mei 1928; La Higuera, Bolivia, 9 Oktoba 1967 ) alikuwa tabibu mzaliwa wa Argentina aliyekuwa mfuasi wa itikadi za Kisoshalisti za Karl Marx. Guevara anajulikana zaidi kwa harakati zake za kimapinduzi dhidi ya tawala za kibepari huko Amerika ya Kusini na Afrika.
Guevara alipewa jina la “che” huko Amerika ya Kati likimaanisha “mshangao”.
Wakati akisomea utabibu, Che Guevara alizunguka katika nchi mbalimbali za Amerika ya Kusini ambapo alijionea mwenyewe umaskini uliokithiri.
