Dimenshia ni kategoria pana ya magonjwa ya ubongo yanayosababisha upunguaji wa muda mrefu na mara kwa mara wa polepole katika uwezo wa kufikiria na kukumbuka kiasi kwamba utendakazi wa kawaida wa mtu unaathiriwa.[1] Dalili zingine zinazotokea sana ni matatizo ya kihisia, matatizo ya lugha, na upungufu katika motisha.[1][2] Ufahamu wa mtu hauathiriwi.[1] Ili utambuzi uweze kufaulu, ni lazima kuwe na mabadiliko kutoka kwa utendakazi wa kawaida wa akili ya mtu na upungufu mkubwa kuliko utokanao na kuzeeka.[1][3] Magonjwa haya pia yana athari kubwa kwa watunzaji wa mtu.[1]