Simba Wanyika ilikuwa bendi nchini Kenya iliyoundwa mwaka wa 1971 na ndugu kutoka Tanzania, Wilson Kinyonga na George Kinyonga. Bendi hii ilivunjika mwaka wa 1994. Simba Wanyika na bendi zingine mbili zilizotoka kwayo, Les Wanyika na Super Wanyika Stars, zilikuwa bendi mashuhuri sana nchini Kenya. Muziki wao uliotokana na sauti ya gitaa, ikiongozwa na mpiga gitaa wa Soukous, Dr Nico,ikichanganywa na maneno matamu ya muziki wa rumba na kuimbwa kwa Kiswahili. Simba wa nyika tafsiri yake kwa Kiingereza ni “Lions of the Savannah”.
